Rugemalira

Kimashami, Kamusiya Kigogo-Kiswahili-Kiingerezai, Rugemalira J., 2008

Kimashami, Kamusiya Kigogo-Kiswahili-Kiingerezai, Rugemalira J., 2008.     

Ingawa kuna maandiko kadhaa katika lugha ya Kimashami, kamusi hii ni ya kwanza kuandaliwa kwa lugha hii. Kamusi yenyewe imekusudiwa kukidhi mahitaji ya wasomaji wa aina mbili. Kwanza, kama ilivyokusudiwa katika mpangilio wa Mradi wa Lugha za Tanzania, itakidhi mahitaji ya watafiti wa isimu wanapofanya uchunguzi kwa kulinganisha data za lugha mbalimbali. Pili, katika jitihada za kukuza na kuhifadhi lugha za Tanzania, kamusi hii itakidhi mahitaji ya msomaji wa kawaida, hasa yule ambaye lugha yake ya kwanza au lugha ya kwanza ya wazazi wake ni Kimashami. Inatazamiwa kwamba kamusi hii itaweka msingi wa kutengeneza kamusi sanifu ya Kimashami, na kuimarisha vigezo vya tahijia na maandishi kwa jumla katika lugha hii.

Kimashami, Kamusiya Kigogo-Kiswahili-Kiingerezai, Rugemalira J., 2008
Скачать и читать Kimashami, Kamusiya Kigogo-Kiswahili-Kiingerezai, Rugemalira J., 2008
 

Cimakonde, Kamusi ya Kimakonde Kiingereza Kiswahili, Rugemalira J., 2013

Cimakonde, Kamusi ya Kimakonde–Kiingereza–Kiswahili, Rugemalira J., 2013.     

Lugha ya Kimakonde inazungumzwa na watu zaidi ya milioni moja na nusu hasa katika mikoa ya Lindi na Mtwara, kusini mwa Tanzania, na pia katika mikoa ya kaskazini mwa Msumbiji. Madhumuni ya kamusi hii ni kuwafikia wazungumzaji wa lugha hii na hivyo kutoa mchango katika kuikuza na kuihifadhi. Ni matumaini yetu kuwa mchango huu utatoa changamoto kwa Wamakonde kutaka kuiboresha kamusi hii na kuitumia kuwafunza vijana matumizi makini ya lugha yao. Pia tunatumaini kwamba wazungumzaji wa lugha nyingine nyingi za Tanzania ambazo hazina maandiko yoyote watahamasika na kuanza kazi ya kuziandika lugha hizi.

Cimakonde, Kamusi ya Kimakonde–Kiingereza–Kiswahili, Rugemalira J., 2013
Скачать и читать Cimakonde, Kamusi ya Kimakonde Kiingereza Kiswahili, Rugemalira J., 2013
 

Cigogo, Kamusiya Kigogo-Kiswahili-Kiingerezai, Rugemalira J., 2008

Cigogo, Kamusiya Kigogo-Kiswahili-Kiingerezai, Rugemalira J., 2008.     

Lugha ya Kigogo inazungumzwa na watu zaidi ya milioni moja hasa katika mkoa wa Dodoma. Ingawa kuna maandiko kadhaa katika lugha ya Kigogo, kamusi hii ni ya kwanza kuandaliwa kwa lugha hii, ukiondoa orodha ya Mwalimu William Mlagulwa yenye maneno 4821. Maandiko mengi yaliyopo yanahusiana na dini ya Kikristu. Jitihada hizo za maandiko ya Biblia zimetoa mchango mkubwa katika kusanifisha lugha hii. Hivyo kamusi hii imefuata kwa karibu taratibu zilizokubalika katika maandiko hayo.

Cigogo, Kamusiya Kigogo-Kiswahili-Kiingerezai, Rugemalira J., 2008
Скачать и читать Cigogo, Kamusiya Kigogo-Kiswahili-Kiingerezai, Rugemalira J., 2008
 





 

2024-12-22 06:41:30